Joy FM
Joy FM
4 February 2026, 13:15

Idara ya uhamiaji Mkoani Kigoma imeendelea na kampeni ya mjue jirani yako inayolenga kuwatambua wahamiaji haramu wanaoingia nchini kinyume cha sheria.
Na Sadick Kibwana
Zaidi ya wahamiaji haramu elfu moja na mia mbili kutoka nchi za Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wameingia nchini pasipo kufata sheria kupitia vipenyo vya mipakani vilivyopo mkoa wa Kigoma kuanzia Desemba 2025 na Januari mwaka huu jambo ambalo linahatarisha usalama wa nchi.
Hayo yamesemwa katika mkutano na wananchi uliofanyika kijiji cha Kaseke, Kata ya simbo Halmashauri ya Wilaya Kigoma Mkoa wa Kigoma na Naibu Afisa Uhamiaji Mkoa Mrakibu Mwandamizi Dominick Kibuga.

Mrakibu Mwandamizi Kibuga amesema idadi ya wanao vuka mipaka bila utaratibu inaendelea kuongezeka hivyo ipo haja ya wananchi kulijua hilo.
Mwenyekiti msaidizi wa Kijiji cha Kaseka, Bwana Denis Nyarusage amesema elimu hiyo inapaswa kutolewa mara kwa mara ili ifahamike zaidi.
Nao baadhi ya Wananchi wameshukuru idara ya Uhamiaji kwa kuwapatia elimu juu ya suala la kuwa na wahamiaji.
Elimu iliyotolewa na Ofisi ya Uhamiaji mkoa wa Kigoma ni mwendelezo wa elimu kwa umma kutolewa ambapo mpaka sasa zaidi ya Vijiji vi4 vimeshafikiwa na kupatiwa elimu hiyo.
