Joy FM
Joy FM
21 January 2026, 14:28

Idara ya uhamiaji Mkoani Kigomma imeendelea na kampeni ya mjue jirani yako yenye lengo la kuwabaini wahamiaji haramu wanaoishi nchini kinyume cha sheria
Na Sadick Kibwana
Wananchi wametakiwa kutoa taarifa za uwepo wa wahamiaji wanaoishi maeneo yao kinyume na sheria za nchi ili raia waweze kufanya shughuli za maendeleo kwa amani na usalama.
Rai hiyo imetolewa na Naibu Afisa Uhamiaji Mkoa wa Kigoma, Dominick Emmanuel Kibuga katika mkutano na wananchi uliyofanyika Kata ya Bitale wilaya ya Kigoma ulioenda sambamba na kaulimbiu inayosema mjue jirani yako.

Amesema usalama wa wilaya ni jukumu la kila raia hasa linapokuja suala la wageni kuingia nchini kinyemela ambao wengi wao hujihusisha na matendo ya uhalifu.
Carson Mzava kutoka Ofisi ya Upelelezi Mkoa amesema kuwepo kwa wahamiaji haramu kumechangia wimbi la uhalifu kuongezeka hivyo ni muhimu kutoa taarifa.
Baadhi ya wananchi walihudhuria mkutano huo wamesema elimu hiyo itolewe mara kwa mara ili jamii iwe na ufahamu.

Wilaya ya Kigoma inazungukwa na nchi za Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo hali inatajwa zaidi ya wahamiaji haramu elfu 4 huvuka mipaka na kuingia nchini na kufanya shughuli za kiuchumi bila kufata utaratibu.