Joy FM
Joy FM
15 January 2026, 11:04

Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, Barbara Dotse amesema shirika hilo linaendelea kutafuta fedha ili huduma za kibinadamu kwa wakimbizi hao wa Congo ziweze kurejea kawaida huku wakitafuta suluhisho la kudumu la wakimbizi hao kurejea nchini mwao.
Na Orida Sayon
Ujumbe wa viongozi wa Serikali ya Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo imetembelea Kambi ya kuwapokea wakimbizi iliyoko Kata ya Kibirizi Manispaa ya Kigoma ujiji na kutoa msaada wa vitu mbalimbali pamoja na chakula.
Ziara hiyo ni mwendelezo wa ziara ya kutembelea wakimbizi kutoka nchini Congo walioko katika kambi za wakimbizi Mkoani Kigoma ikiongozwa na Waziri anayeshughulikia masuala ya ustawi wa jamii, hatua za kibinadamu na mshikamano Eve Masudi .

Mhe. Eve Masudi ametumia ziara hiyo kuishukuru shirika la umoja wa Mataifa linaloshughulikia wakimbizi UNHCR kwa kuwatunza wakimbizi na kumpongeza Rais wa Tanzania kuwa kiongozi bora mwanamke na mfano wa kuigwa na wanawake viongozi Afrika.
Akizungumza kwa niaba ya Serikali ya Tanzania, Naibu Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki, James Millya amesema Tanzania inajali wakimbizi waliokimbia hali ya vurugu nchini kongo na inaendelea kuiombea ili iweze kurejea katika amani.

Kwa upande wake, Mwakilishi Mkaazi wa shirika la umoja wa Mataifa linaloshughulikia wakimbizi UNHCR Tanzania Bi. Barbra Dotse ameishukuru Tanzania na Congo kwa ushirikiano wanatoa kwa shirika hilo hasa kuwajali wakimbizi.
Baadhi ya wakimbizi wakawa na haya ya kueleza kwa viongozi wao toka kongo na Tanzania.