Joy FM
Joy FM
6 January 2026, 14:21

Wananchi Mkoani Kigoma wametakiwa kuendelea kutoa taarifa za watu wanaingia na kuishi Nchini kinyume cha sheria ili waweze kuchukuliwa hatua za kisheria
Na Orida Sayon
Jeshi la uhamiaji Mkoani Kigoma limesema limeanza mkakati wa kudhibiti uhamiaji haramu kutoka nchi jirani za Kidemokrasia ya kongo (DRC) na Burundi ujulikanao kama mjue jirani yao.
Hayo yamebainishwa na Naibu Afisa uhamiaji mkoa wa kigoma Mrakibu Mwandamizi Dominick Emmanuel Kibuga wakati akizungumza na Joy fm ambapo amesema kufuatia madhara yaliyobainishwa katika operesheni zilizofanyika mwaka 2025 zimepelekea kuja na mkakati madhubuti utakaosaidia kudhibi wahamiaji haramu kuingia nchini.

Amesema miongoni mwa mikakati hiyo ni pamoja na kuimarisha doria kwenye maeneo yenye shughuli zinzohitaji vibarua, kupata rekodi kupitia kwa viongozi wa serikali za mitaa na kuboresha huduma kwenye vituo vya pembezoni mwa barabara.
Afande Kibuga amesema katika doria na oparesheni zilizofanyika kuanzia januari hadi disemba mwaka 2025 jeshi la uhamiaji lilifanikiwa kukamata takribani wahamiaji haramu 5881 na kuwataka wananchi kuendelea kushiriki kutoa taarifa za wageni wanaoingia nchini kinyume cha sheria.
