Joy FM
Joy FM
17 November 2025, 08:56

Mkoa wa Kigoma umeanza rasmi utekelezaji wa ujenzi wa masoko pembezoni mwa barabara umeanza ili kuhakikisha wajasiriamali wanapata sehemu ya kuuzia.
Na Mwandishi wetu
Serikali mkoani hapa inatekeleza mradi wa ujenzi wa masoko madogo 14 yenye Thamani ya Shilingi Mil.490 kwa ajili ya wajasiriamali wanaofanya biashara ndogondogo pembezoni mwa barabara kuu ili kuwapatia mazingira rafiki kibiashara.

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Balozi Simon Sirro ameishukuru Serikali kwa kushirikiana na mdau wa Maendeleo, Shirika la Maendeleo la watu wa Ubelgiji (Enabel) kwa kutekeleza mradi, huku akiwataka wanufaika kuitunza miundombinu hiyo ili iweze kutumika kwa muda mrefu baada ya kukabidhiwa.
Upande wake Katibu Tawala Mkoa wa Kigoma Hassan Rugwa amesema wanufaika wa masoko hayo ni wafanyabiashara wadodo wanaoendesha shughuli zao katika stendi ndogo zilizopo pembezoni mwa barabara katika maeneo ya Rusesa, Kasangezi, Nkundutsi, Bugaga, Machazo, Mlangala, Mkongoro na Kakonko.
Amesema serikali ya mkoa imeingia mkataba na Mkandarasi Lilangela Construction Co. Ltd na Ufahamu Women Group wote wa Kigoma, kutekeleza