Joy FM

Dkt. Mpango ashiriki zoezi la upigaji kura Buhigwe

29 October 2025, 10:01

Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango akiwa anaweka karatasi ya kura kwenye sanduku baada ya kupiga kura, Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango ameshiriki zoezi la kupiga kura ya kuchagua Rais, Mbunge na Diwani akiwa katika Kijiji cha Kasumo, Wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma leo tarehe 29 Oktoba 2025.

Na Michael Mpunije

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Philipe Mpango amewashukuru wananchi wa kijiji cha Kasumo wilayani Buhigwe Mkoani kigoma kwa kujitokeza kupiga kura katika uchaguzi Mkuu wa Rais,wabunge na madiwani leo Oktoba 29,2025.

Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango akipiga kura kituo cha Kasumo Buhigwe, Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais

Akizungumza muda mfupi baada ya kushiriki zoezi la Kupiga kura Dkt.Mpango amesisitiza wananchi kujitokeza kwa wingi kutimiza haki yao ya kikatiba kuwachagua viongozi wanaowataka.

Dkt Mpango amesisitiza kudumisha amani katika kipindi chote cha uchaguzi ambapo amewashukuru wananchi wa kijiji cha Kasumo kata ya kajana wilayani Buhigwe kwa kujitokeza kwa wingi kupiga kura.

Sauti ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Philipe Mpango
Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango akiwa kwenye mstari na wananchi wengine akisubiri kupiga kura, Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais

Kwa upande wao baadhi ya wananchi wa kijiji cha Kasumo wilayani Buhigwe ambao wamejitokeza kupiga kura wamepongeza seriakli kwa kuimarisha hali ya ulinzi na usalama na kupelekea uchaguzi huo kufanyika kwa amani na utulivu.