Joy FM

Kandahari kuanzisha mfuko kusaidia wenye ulemavu Uvinza

23 October 2025, 15:30

Mgombea ubunge jimbo la Kigoma kusini akizungumza na mzee mwenye ulemavu wakati wa kampeni, Picha na Jacob Ruvilo

Watu wenye ulemavu wameomba jamii kutoendelea kuwanyanyapaa badala yake wawaelekeze na kuwasaidia ili nao waweze kufanya shughuli za kuwaingizia kipato na kuchangia pato la familia na Taifa

Na Mwandishi wetu
Mgombea ubunge Jimbo la Kigoma kusini Nuru Kashakali maarufu Kandahari ameahidi kuona uwezakano wa kuanzisha mfuko rasmi wa kusaidia na kuwezesha watu wenye ulemavu katika jimbo hilo kiuchumi.

Kauli ya Mgombea huyo ameitoa akiwa Kijiji cha Uvinza katika mkutano wa kampeni kufuatia mmoja wa walemavu Aziz Ally kuomba msaada akilalamika jamii ya walemavu kutengwa nakunyanyapaliwa kiuchumi.

Mgombea ubunge jimbo la Kigoma kusini akizungumza na mzee mwenye ulemavu wakati wa kampeni, Picha na Jacob Ruvilo

Kandahari amesisitiza kuwa walemavu wakiwezeshwa wanaweza kuzalisha mali na kumudu maisha yao na kuongeza pato kwa nchi badala ya kutelekezwa na kubaki kuwa omba omba.

Kandali amesisitiza kuwa adhima yake kubwa ni kuwasaidia walemavu kuishi maisha ya staha kama ambavyo amepanga kutoa mikopo kwa makundi mengine ya vijana na akina mama nakwamba yote atatekeleza mara atakaposhinda kiti cha Ubunge.

Kandahari alifanya mikutano mingine eneo la Kata ya Basanza, kata ya Uvinza katika vijiji vya Chakulu na Lugufu Wilayani Uvinza Mkoani Kigoma

Mgombea ubunge jimbo la Kigoma kusini akizungumza na mzee mwenye ulemavu wakati wa kampeni, Picha na Jacob Ruvilo