Joy FM
Joy FM
12 September 2025, 13:23

Mgombea Uras kupitia chama cha mapinduzi CCM, Dkt. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwasili Mkoani Kigoma kwa ajili kampeni za kuomba kura kwa wananchi
Na Esperance Ramadhan
Mkuu wa Wilaya Kigoma Dk. Rashid Chuachua amewataka wananchi wa Mkoa Kigoma kujitokeza kwa wingi kumpokea na kumuonyesha upendo Rais Samia Suluhu Hassan ambaye atafanya ziara ya siku mbili mkoani Kigoma kuanzia tarehe 13 mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, Mkuu huyo wa Wilaya Kigoma amesema kuwa Rais Samia ataingia Mkoani Kigoma Septemba 12 akitokea mkoani Tabora ambapo tarehe 13 Agosti atafanya mikutano katika wilaya za Uvinza, Kasulu na Buhigwe.
Dk. Chuachua amesema kuwa tarehe 14 Rais Samia atafanya mkutano mkubwa wa kampeni katika viwanja vya Katosho Manispaa ya Kigoma Ujiji ambapo amewataka wananchi wote kujitokeza kwa wingi kusikiliza sera, ilani na mambo ambayo serikali imeyafanya lakini pia ataeleza mipango ambayo serikali yake itafanya kwa miaka mitano ijayo.
Kwa upande wake, Katibu wa CCM Wilaya ya Kigomaa, Sadiki Kadulo akizungumza na Waandishi wa habari ujio wa Rais Samia mkoani Kigoma alisema kuwa wanatarajia kufanya mkutano mkubwa ambao utavunja rekodi ya watu watakaohudhuria hivyo amewataka kuja kusikiliza mambo ambayo kiongozi huyo amekuja nayo.
Kadulo amesemaa kuwa Rais Samia amefanya makubwa makubwa katika miaka yake minne aliyokuwa Rais wa nchii na kwa mkoa Kigoma ipo miradi mingi na mikubwa ambayo imefanya hivyo wananchi wanapaswa kujitokeza kusikiliza mambo gani mapya ambayo kiongozi huyo amekuja nayo.
Amesema kabla ya mkutano huo kutakuwa na matembezi ya upendo ambayo yatahudhuriwa na makundi mabalimbali yakiwemo makundi ya ujasiriamali ili kuenzi kazi zilizofanywa katika kipindi cha serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluh Hassan.
Baadhi ya wananchi Mjini Kigoma wameeleza hisia zao kuhusu ujio wa Dkt. Samia Suluhu Hassan Mkoani Kigoma.
Mkutano huo wa mgombea Urais kupitia chama cha mapinduzi CCM utafanyika septemba 14, katika Bandari kavu ya Katosho.
