Joy FM

Serukamba aahidi neema kwa wananchi Kigoma Kaskazini

1 September 2025, 13:31

Mgombea ubenge Jimbo la Kigoma Kaskazini Peter Serukamba akiwa katika kampeni katika uwanja wa Kazegunge, Picha na Tresiphol Odace Bwana

Mgombea Ubunge Jimbo la Kigoma Kaskazini Peter Serukamba na Mgombea udiwani Kata ya Mungonya Agustino Mbanga wamesema watahakikisha wanatekeleza miradi ya maendeleo kwa wananchi wa Kata ya Mungomya ikiwemo barabara, maji na afya.

Na Tresiphol Odace Bwana – Kigoma

Wananchi  wa Kata ya Mungonya Halmashauri ya Wilaya Kigoma wameeleza kuwa miongoni mwa mambo ambayo wanatamani wagombea wa nafasi ya udiwani na Ubunge watakapochaguliwa waweze kuyashughulikia kuwa ni pamoja na ukosefu wa maji safi na salama, barababara na huduma za afya.

Wakizungumza na Redio Joy Fm, Baadhi ya wananchi wa maeneo ya Kazegunga, Msimba na Kamala wamesema kata hiyo inakabiliwa na changamoto za ukosefu wa barabara za uhakika na kusababisha shughuli za usafiri kuwa ngumu hasa wakati wa kusafirisha akina mama wajawazito.

Sauti ya baadhi ya wananchi wa maeneo ya Kazegunga, Msimba na Kamala

Haya yote yanajili ikiwa ni siku chache baada ya uzinduzi wa kampeni za uchaguzi Mkuu kwa vyama vyote kuzinduliwa Agosti 28 ambapo tayari wagombea wanaendelea kunadi sera zao na hapa Mgombea udiwani Kata ya Mungonya Bw. Agustino Mbanga anaeleza kuwa atahakikisha anashirikiana na wananchi katika kushughulikia changamoto hizo.

Sauti ya Mgombea udiwani Kata ya Mungonya Bw. Agustino Mbanga
Mgombea ubingwa Peter Serukumba na Mgombea udiwani Agustino Mbanga wakiwa jikwaaani kuomba ridha ya wananchi kuchaguliwa, Picha na Tresipholi Odace Bwana

Kwa upande wake, Mgombea ubunge Jimbo la Kigoma Kaskazini Peter  Joseph Serukamba akizungumza katika mkutano wa kampeni katika uwanja wa Kazegunga amesema miongoni wa vipaumbele vyake ni kuhakikisha anatekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo kwa wananchi ikiwemo suala la afya na barabara.

Sauti ya Mgombea ubunge Jimbo la Kigoma Kaskazini Peter  Joseph Serukamba

Kampeni za uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 zinaendele katika maeneo mbalimbali nchini Tanzania na uchaguzi wa Rais, Ubunge na Madiwani unatarajia kufanyika oktoba 29 mwaka huu.