Joy FM
Joy FM
27 August 2025, 16:36

Vijana waliohitimu mafunzo ya awali ya Jeshi la akiba wameaswa kuwa wazalendo
Na Lucas Hoha
Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Dkt Rashird Chuachua amewataka vijana waliohitimu mafunzo ya awali ya jeshi la akiba kuwa wazalendo katika kulinda na kuhakikisha nchi yao inakuwa salama na kukataa maovu yanayofanywa watu wasio waaminifu.
Katika hafla ya kufunga mafunzo ya awali kwa wahitimu wa mafunzo ya jeshi la akiba ambayo yamefanyika katika uwanja wa lake Tanganyika uliopo Manispaa ya Kigoma Ujiji, Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Dkt Rashid Chuachua pamoja na mambo mengine amewataka askari kuwa waaminifu katika kuwatumikia watanzania.
Naye Katibu tarafa wa Kigoma kusini Dahaye Anney amewaomba vijana waliopo mtaani kujiunga na mafunzo ya jeshi la akiba.
Awali akisoma lisala kwa niaba ya wahitimu wa mafunzo Philipo James amesema katika mafunzo hayo wamejifunza vitu mbalimbali ikiwemo utiifu, huku wakiomba kupewa kipaumbele katika shughuli mbalimbali za serikali.
Mafunzo ya askari hao yamedumu kwa miezi 4 na kwa mjibu wa lisala jumla ya wahitimu 116 wamemaliza mafunzo hao.
