Joy FM
Joy FM
5 August 2025, 13:08

Jeshi la Polisi Mkoani Kigoma limethibitisha watu watatu wanaosadikiwa kuwa Majambazi kuuawa katika tukio la majibizano ya risasi katika jaribio la kutaka kuteka magari eneo la Kumshindwi Wilayani Kibondo Mkoani Kigoma.
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Kigoma Filemon Makungu amesema katika tukio hilo wamekamata silaha mbalimbali ikiwemo Bunduki moja aina ya Ak 47, magazine moja , risasi kumi pamoja na silaha za jadi.
Kufuatia tukio hilo, wananchi wameomba Jeshi la Polisi kuongeza nguvu kudhibiti matukio ya ujambazi na kufanya mkoa wa Kigoma kuwa shwari bila hofu.
Miili ya watu waliouawa bado haijatambuliwa na hivyo kuhifadhiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Kibondo huku wengine waliokimbia katika tukio hilo wakiendelea kusakwa na Jeshi la Polisi.