Joy FM
Joy FM
5 August 2025, 12:26

Misako mbalimbali ya kuwabaini na kuwakamata wahamiaji haramu wanaoingia nchini kinyume cha sheria imeendelea katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Kigoma
Jumla ya wahamiaji haramu 793 kutoka mataifa ya Burundi, Congo, Rwanda na Uganda wamekamatwa na Idara ya Uhamiaji Mkoani Kigoma wengi wao wakiwa wanafanya kazi za uzalishaji mali hasa kilimo na Uvuvi wakiwa hawana nyaraka zinazowapa kibali cha kufanya kazi na kukaa nchini.