Joy FM
Joy FM
4 August 2025, 15:48

Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Kasulu Mjini, Nurfus Aziz, amewatakiwa wasimamizi kuhakikisha vituo vya kupiga kura vinafunguliwa mapema kulingana na maelekezo ya tume huru ya taifa ya Uchaguzi
Na Hagai Ruyagila
Wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya kata katika Halmashauri ya Mji wa Kasulu Mkoani Kigoma wametakiwa kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa na tume huru ya taifa ya Uchaguzi ili kuepuka kuwa chanzo cha malalamiko kutoka kwa vyama vya siasa.
Akizungumza wakati wa zoezi la kutoa mafunzo na kuwaapisha wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi mkuu kutoka kata 15 za Halmashauri ya Mji Kasulu Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Kasulu Mjini, Nurfus Aziz, amesema wasimamizi hao wanatakiwa kuhakikisha vituo vya kupiga kura vinafunguliwa mapema kulingana na maelekezo ya tume huru ya taifa ya Uchaguzi.

Aidha bw. Aziz amesisitiza kuwa jukumu la kusimamia uchaguzi ni la heshima na dhamana kubwa, hivyo linahitaji uadilifu, uaminifu na uzingatiaji wa taratibu zote za uchaguzi.
Afisa uchaguzi halmashauri ya Mji wa Kasulu Daniel Kaloza amesema Tume ya Taifa ya Uchaguzi ina imani kubwa na wasaidizi wake, hivyo ni wajibu wao kuhakikisha kila hatua ya uchaguzi inatekelezwa kwa weledi na kwa manufaa ya taifa.

Baadhi ya wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi wamesema wako tayari kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu na kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa huru na haki ili viongozi watakao chaguliwa wanaweza kutekeleza majukumu yao kulingana na matakwa ya wananchi waliowachagua.
Insert 03 ……. Wasimamizi wasaidizi wa