Joy FM

Viongozi wafuatilie njia za wahamiaji kuingia Nchini

18 July 2025, 11:22

Mrakibu Msaidizi wa uhamiaji na Naibu Afisa Uhamiaji mkoa wa Kigoma Dominick Emmanuel Kibuga, Picha na Hamis Ntelekwa

Viongozi wa Serikali za vijiji na mitaa wameshauriwa kutoa taarifa na njia zinazotumiwa na wahamiaji haraumu wanazotumia kuingia nchini kunyume cha sheria

Na Orida Sayon

Wananchi Mkoani Kigoma wameomba Serikali kupitia ofisi ya uhamiaji kushirikiana na viongozi wa ngazi za vijiji na mitaa ili kubaini njia zinazotumiwa wahamiaji haramu kuingia nchini.

Hayo yanajiri ikiwa ni siku chache ofisi ya uhamiaji Mkoani Kigoma kuendesha oparesheni na kuwakamatwa wahamiaji haramu zaidi mia tisa waliokuwa wakiishi nchini kinuyume na sheria.

Sauti ya Wananchi Mkoani Kigoma

Mrakibu Msaidizi wa uhamiaji na Naibu Afisa Uhamiaji mkoa wa Kigoma Dominick Emmanuel Kibuga amebainisha kuwa mahusiano kati ya wenyeji na wageni imekua sababu ya uwepo wa wahamiaji haramu mkoani hapa.

Sauti ya Mrakibu Msaidizi wa uhamiaji na Naibu Afisa Uhamiaji mkoa wa Kigoma Dominick Emmanuel Kibuga

Aidha Kibuga ametoa wito kwa wananchi hasa walio mpakani kutoa taarifa za wahamiaji haramu ili kuondokana na mrundikano wa wageni wasiotambulika kisheria.

Sauti ya Mrakibu Msaidizi wa uhamiaji na Naibu Afisa Uhamiaji mkoa wa Kigoma Dominick Emmanuel Kibuga

Mkoa wa Kigoma ni miongoni mwa mikoa iliyo mipakani mwa Tanzania ikiwa imepakana na Taifa la Burundi na Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo huku ikiwa na mwingiliano mkubwa wa wageni hali inayosababisha baadhi yao kuingia mkoani hapa kiholela na hivi karibuni ofisi ya uhamiaji mkoani Kigoma
imeendesha misako nad doria ambapo juni 1-julai 8 2025 ili kamata wahamiaji haramu 926, na tarehe 8-14 julai wakiwa wahamiaji haramu 419 hali hii ikionyesha kuwa na namba kumbwa ya wahamiaji haramu wanaoingia nchini.