Joy FM
Joy FM
8 July 2025, 16:11

Viongozi wa Serikali za mitaa na vijiji Mkoani Kigoma wametakiwa kufuatilia na kutoa taarifa za watu wanaoingia kwenye maeneo yao ili kujua kama ni wahamiaji haramu.
Na Lucas Hoha
Idara ya uhamiaji Mkoa wa Kigoma kupitia misako mbalimbali iliyofanyika June 2025 imefanikiwa kuwakamata wahamiaji haramu 926 wakiwa na makosa mbalimbali ikiwemo baadhi yao kuingia nchini bila kufuata sheria ambapo raia 706 kati ya hao wanatoka katika nchi ya Burundi.
Hayo yamesemwa na Afisa Uhamiaji Mkoa wa Kigoma Dismas Mlula wakati akizungumza na waandishi wa habari ili kutoa taarifa ya mafanikio ya misako inayofanyika ya watu ambao wanaishi nchini kinyume na sheria.
Wakati huohuo, Mlula amewaomba raia wa kigeni wanaokuja nchini Tanzania kwa ajili utafutaji wa halali kufuata utaratibu wa kisheria kabla yakuingia nchini na kuwataka wenyeviti wa Vijiji na watendaji wa kata kutoa tarifa kwa idara ya uhamiaji kuhusu wahamiaji haramu ili kulinda amani iliyopo.
Aidha Idara ya uhamiaji imekemea tabia ya baadhi ya raia wa Tanzania kujihusisha na usafirishaji wa binadamu kutoka nchi moja kwenda nchi nyingine na kuwataka kuacha tabia hiyo.