Joy FM
Joy FM
12 May 2025, 12:54

Viongozi wa dini na jamii wameaswa kuliombea Taifa dhidi ya matukio yanaendelea kwenye jamii ambayo yanaweza kuleta uvunjifu wa amani.
Na Tryphone Odace
Askofu wa Jimbo Katoliki la Kigoma Joseph Mlola amewataka waumini wa kanisa hilo na watanzania kwa ujumla kuelendelea kuliombea Taifa hasa kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi Mkuu utakaofanyika mwezi Oktoba 2025.
Askofu Joseph Mlola amesema hayo wakati wa misa iliyofanyika katika Parokia ya Mtakatifu Maria mama wa Mungu Kibondo iliyoambatana na harambe ya ujenzi wa kanisa kubwa la kisasa parokiani hapo.

Amesema kumekuwa matukio mengi kwenye jamii ambayo yanakatisha tama jambo ambalo linahatarisha amani na utulivu wa jamii na taifa kwa ujumla.
Katika harambe hiyo, Mgeni rasmi alikuwa ni Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Reli Nchini TRC, Masanja Kadogosa amesema taifa liko katika kipindi cha uchaguzi na hivyo jamii haina budi kuhubiri amani kwa ajili ya kizazi kijacho.
Aidha katika harambe hiyo iliyoendeshwa na Mkurugenzi wa TRC Masanja Kadogosa zaidi ya shilingi milioni mia mbili hamsini zimepatikana ili kuendelea na ujenzi wa kanisa hilo.
Baadhi ya waumini wakatoliki Parokia ya Mtakatifu Maria mama wa Mungu Kibondo wamesema suala la amanai ni muhimu huku wakipongeza harambe hiyo kwani itasaidia kuongeza sehemu ya kusalia.