

31 January 2025, 12:11
Madiwani katika Halmashauri ya Manispaa ya Geita wamesema bajeti hiyo itaenda kusaidia katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa wananchi
Na Samwel Masunzu – Geita
Baraza la madiwani la halmashauri ya manispaa ya Geita mkoani Geita limepitisha rasmu ya makadirio ya bajeti ya kiasi cha shilingi bilioni 68.3 kwa mwaka wa fedha wa 2025/26
Bajeti hiyo imepitishwa kupitia kikao cha baraza hilo ambacho kimefanyika eneo la uwekeza EPZA Bombambili mjini Geita
Mkurugenzi mtendaji wa manispaa ya Geita bw. Yefred Myenzi amesema bajeti hiyo ni ongezeko la asilimia 13.2 ya bajeti ya mwaka 2024/25 na watahakikisha wanadhibiti ukwepaji wa ulipaji wa kodi kupitia vyanzo vya mapato vilivyokuwepo na vile vilivyoongezeka.
Kwa upande wake kaimu mstahiki meya wa manispaa ya Geita Elias Ngole amesema bajeti hiyo itasaidia kuendelea kuongeza ukarabati wa miundombinu ikiwemo barabara na kufungua miradi mipya ya halmashauri.