Naibu Waziri Mkuu awawashia moto wakandarasi umeme Kigoma
20 September 2024, 09:31
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mheshimiwa Dkt. Dotto Biteko, ameagiza wakandarasi wa ujenzi wa miradi ya kimkakati ya umeme mkoani Kigoma, kuongeza kasi ya utekelezaji ili miradi hiyo ikamilike kwa wakati na kusaidia katika kukuza uchumi wa watanzania na taifa.
Akihutubia mamia ya wakazi wa mkoa wa Kigoma mara baada ya kuweka mawe ya msingi katika miradi mitatu ya umeme Kigoma, ikiwemo mradi wa uzalishaji umeme katika mto Malagarasi, njia kuu ya kusafirisha umeme wa Gridi ya Taifa kutoka Nyakanazi na Kituo cha kupoza umeme Kidakhwe, Mh. Naibu Waziri Mkuu Dkt. Dotto Biteko, amesema miradi hiyo isaidie katika uwekezaji wa viwanda na kukuza uchumi Kwa wananchi.
Akitoa taarifa ya miradi ya umeme wa gridi ya taifa, Mkurugenzi Mtendaji Shirika la Umeme Tanesco Gissima Nyamahanga amesema miradi hiyo kukamilika kwake itakuwa chachu ya kuuza umeme hadi nchi jirani, huku viongozi wengine akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye wakieleza tija katika uwekezaji wa viwanda.