Joy FM

Wakandarasi REA wanyoshewa kidole Kigoma

20 September 2024, 08:58

Bodi ya Nishati Vijiji REB, Imewaonya wakandarasi wanaosusua kukamilisha miradi ya Wakala wa Nishati Vijijini  REA, ikisisitiza miradi ikamilike kwa wakati katika vijiji vyote vinavyotekeleza miradi nchini, na kusaidia wananchi kupata nishati ya umeme kwa wakati.

Bodi ya Nishati Vijiji REB, imezuru katika miradi inayotekelezwa mkoani Kigoma, katika wilaya za Uvinza na Manispaa ya Kigoma Ujiji, ambapo wananchi wameeleza tija ya miradi hiyo na kuomba ikamilike kwa wakati.

Sauti za wananchi wa Wilaya ya Uvinza na Manispaa ya Kigoma Ujiji.

Mkurugenzi mkuu Wakala wa Nishati Vijiji Mhandisi Hassan Saidy amesema vijiji 92 vinaenda kupata nishati ya umeme na kumaliza vijiji vyote 306 kuwa na nishati hiyo kwa mkoa wa Kigoma,  wakati Mwenyekiti wa Bodi,  Bodi ya nishati Vijijini Barozi Meja Jeneral mstaafu Jacobu Kingu akisisitiza wakandarasi kutekeleza miradi kulingana na makubaliano ya mikataba.