Joy FM

Maafisa ugani watakiwa kuwatembelea wakulima Kigoma

19 August 2024, 16:42

Mkuu wa Mkoa Kigoma akikabidhi ufunguo wa gari kwa mwakilishi wa maafisa ugani mkoani kigoma wakati hafla ya kugawa vitendea kazi kwa maafisa ugani, Picha na Tovuti ya Mkoa

Mkuu wa Mkoa Kigoma Kamishna Jenerali mstaafu wa jeshi la zimamoto na uokoaji Thobias Andengenye amewataka maafisa ugani kuwatembelea maafisa ugani na kusikiliza kero zinazowakabili kwenye shughuli za kilimo na kuzitatua.

Na Tryphone Odace – Kigoma

Kutatuliwa kwa Changamoto ya kukosekana kwa usafiri wa uhakika iliyokuwa ikiwakabili Maafisa Ugani katika maeneo mbalimbali Nchini, imesaidia kuboresha sekta ya kilimo na kuongeza tija ya uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara mkoani Kigoma.

Mkuu wa Mkoa Kigoma akikabidhi vitendea kazi kwa maafisa ugani, Picha na Tovuti ya Mkoa Kigoma

Wakizungumza na kituo hiki baadhai ya maafisa ugani mara baada ya kupokea vitendea kazi mbalimbali vilivyotolewa na serikali, wameeleza kuwa awali walikuwa wanakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa usafiri ili kuwafikia wakulima kwa urahisi lakini kwa sasa changamoto hiyo imetatuliwa.

Sauti ya maafisa ugani mara baada ya kupokea vitendea kazi mbalimbali vilivyotolewa na serikali

Akikabidhi magari na vitendea kazi vingine kwa ajili ya maafisa ugani na watendaji wengine wa idara ya kilimo mkuu wa mkoa wa kigoma Thobias Andengenye amewataka kutumia zana hizo kutatua matatizo yanayowakabili wakulima na kuongeza tija ya uzalishaji.

Sauti ya mkuu wa mkoa wa kigoma Thobias Andengenye

Hata hivyo amewataka kutunza vitendea kazi hivyo vikiwemo magari, pikipiki na sale maalumu zilizotolewa kwa maafisa ugani ili kuwatambulisha kwa wakulima katika vituo vyao vya kazi.