Joy FM

Madereva watakiwa kutii sheria za barabarani

7 August 2024, 13:32

SGT Sabato Rajabu mwakilishi wa afande DTO wilaya ya Kasulu, Picha na Hagai Ruyagila

Jeshi la polisi wilayani kasulu mkoani kigoma limewataka madereva wa vyombo vya moto na watumiaji wa barabara kuzingatia matumizi ya barabara ili kuepukana na ajali zinazojitokeza wakiwa barabarani.

Na Hagai Ruyagila – Kasulu

Watumiaji wa vyombo vya moto hususani waendesha pikipiki wilayani Kasulu Mkoani Kigoma wametakiwa kujali na kutii sheria za usalama barabarani wanapo kuwa katika safari zao ili kuepukana na ajali.

Wito huo umetolewa na SGT Sabato Rajabu mwakilishi wa afande DTO wilaya ya Kasulu wakati akizungumza na radio joy fm katika chuo cha uwalimu kilichopo mjini Kasulu.

Amewasisitiza madereva wote wa vyombo vya moto kuzijua sheria za usalama barabarani ili kuepuka kuwa chanzo cha ajali kufuatia ajali nyingi kutokea kwa kutokujali sheria barabarani.

Sauti ya SGT Sabato Rajabu mwakilishi wa afande DTO wilaya ya Kasulu

Kwa upande wake Mchungaji wa kanisa la angikana Ujiji Canon Anderson Bilasa akiwakilisha viongozi wa dini ameishauri serikali kutumia siku za ibada kwa ajili ya kuelimisha jamii namna bora ya uendeshaji wa vyombo vya moto ili kuepusha ajali zinazo jitokeza.

Sauti yaMchungaji wa kanisa la anglikana Ujiji, Canoni Anderson Bilasa

Nao baadhi ya waendesha vyombo vya moto kutoka wilayani Kasulu Mkoani Kigoma wameiomba serikali kuendelea kuwaelimisha kuhusu sheria za usalama barabarani.

Sauti za waendesha vyombo vya moto ksulu

Kikosi cha usalama barabarani kimeundwa mwaka 1975 toka ndani ya jeshi la polisi baada ya kuona ajali nyingi zinatokea nchini