Wananchi watakiwa kutunza vyanzo vya maji Buhigwe
30 July 2024, 11:42
Serikali wilayani Buhigwe mkoani kigoma imesema itaendelea kutoa elimu ya utunzaji wa mazingira yanayozunguka vya maji ili kusaidia kuhifadhi vyanzo vya manufaa ya jamii nzima.
Na Michael Mpunije – Buhigwe
Wananchi wilayani Buhigwe Mkoani Kigoma wametakiwa kutunza vyanzo vya maji ili viweze kudumu kwa muda mrefu kutokana na baadhi yao kuwa chanzo cha uharibifu wa vyanzo hivyo.
Shughuli za kilimo karibu na vyanzo vya maji ni miongoni mwa masuala ambayo huchangia katika uchafuzi wa maji pamoja na uharibifu wa vyanzo vya maji jambo ambalo linakemewa na serikali
Meneja wa Ruwasa wilaya ya Buhigwe injinia Golden gwa katoto amesema kukosekana kwa elimu ya utunzaji wa vyanzo vya maji kwa wananchi wilayani huo umeonekana kuwa changamoto kwakuwa wengi wao wamekuwa wakifanya shughuli za kibinadamu katika vyanzo vya maji ambapo anatoa wito kwa jamii kutunza miradi hiyo.
Sambamba na hayo injinia Golden amesema serikali imelenga kutatua kero ya uhaba wa maji wilayani Buhigwe ambapo baadhi ya miradi ya maji inaendelea kujengwa wilayani humo sanjari na kusisitiza wananchi kuwa walinzi wa miradi hiyo na kuhakikisha wanatunza vyanzo vya maji ili viweze kuwaondolea usumbufu wa kufuata huduma ya maji umbali mrefu.