Joy FM

Wafanyabiashara watakiwa kutumia vifaa vya kuzimia moto

28 June 2024, 12:32

Ni muonekano wa mitungi ya gesi ya kuzima moto yanapotokea majanga ya moto, Picha na mtandao

Jeshi la zimamoto na uokoaji wilayani kasulu mkoani kigoma limesema wafanyabiashara na jamii kwa ujumla hawana budi kutumia vifaa vya kuzima moto hasa kwenye nyumba zao ili kusaidia pale majanga yanapotokea.

Na Michael Mpunije – Kasulu

Wafanyabiashara wilayani Kasulu Mkoani Kigoma wametakiwa kuwa na vifaa vya kuzimia moto katika maeneo yao ya kazi ili kukabaliana na majanga ya moto yanayoweza kujitokeza na kusababisha madhara.

Akizungumza na Radio Joy Mkuu wa jeshi la zimamoto na uokoaji Wilaya ya Kasulu Insipekta Anthony Marwa amesema ili kukabiliana na majanga ya moto wafanyabiashara wanatakiwa kukagua mifumo ya umeme ya nyumba zao ambayo imekuwa chanzo cha majanga ya moto.

Insepekta marwa amesema ni muhimu kuwa na vifaa vya kuzimia moto kwenye maeneo ya kazi ili kudhibiti majanga ya moto yanapotokea yasiweze kusababisha madhara.

Sauti ya Mkuu wa jeshi la zimamoto na uokoaji Wilaya ya Kasulu Insipekta Anthony Marwa

Aidha insipekta Marwa ameongeza kuwa wameanza kutoa hati za usalama kwa wafanya biashara pamoja na kuwataka wananchi kutoa taarifa za mapema pindi majanga ya moto yanapotokea.

Hata hivyo baadhi ya wafanyabiashara wa soko kuu la kumsenga mjini Kasulu wamesema baadhi ya wananchi hawana elimu kuhusu matumizi ya vifaa vya kuzimia moto na kuomba jeshi la zimamoto na uokoaji kuendelea kutoa elimu kwa wananchi wote pamoja na kufika kwa wakati eneo la tukio pindi matukio ya moto yanapotokea. 

Ni muonekano wa mitungi ya gesi ya kuzima moto yanapotokea majanga ya moto, Picha na mtandao