Joy FM

Kumbi za video chanzo cha ukatilii na ulawiti watoto

12 June 2024, 08:27

Baadhi ya vijana wakiwa katika mkutano wa hadhara, Picha na Mwandishi wetu

Jamii wilayani kasulu imetakiwa kushirikiana na serikali, wadau na wazazi kudhibiti watoto kutoenda sehemu za sterehe ikiwemo kwenye vibanda vya video ili kupunguza kufanyiwa ukatilii.

Na Michael Mpunije – Kasulu

Wazazi na walezi wilayani Kasulu mkoani Kigoma wametakiwa kudhibiti watoto wao kuingia katika kumbi za video na kuwaepusha kutembea usiku  jambo ambalo limetajwa kuwa chanzo cha vitendo vya ukatili na ulawiti dhidi ya wanawake na watoto.

Wito huo umetolewa na Mganga Mkuu wa halmashauri ya mji kasulu dokta,Peter janga wakati akizungumza na wazazi pamoja na viongozi wa serikali za mitaa katika mafunzo ya kupinga ukatili wa kijinsia yaliyofadhiliwa Shirika la kimataifa la IRC.

Dkt.Janga amesema takwimu za vitendo vya ulawiti katika halmashauri ya mji kasulu vinazidi kupanda ingawa amebainisha kuwa kuna uwezekano mkubwa takwimu hizo zikashuka ikiwa wazazi na walezi wataamua kulivalia njuga suala hilo na kuhakikisha vitendo hivyo vinakomeshwa kwa kutoa ushirikiano kwa kwa jeshi la polisi.

Sauti ya Mganga Mkuu wa halmashauri ya mji kasulu dokta, Peter janga

Aidha ameongeza kuwa jamii inatakiwa kudhibiti baadhi ya vyanzo ambavyo vimeonekana kuchangia katika vitendo vya ukatili ikiwa ni pamoja na wazazi kuwaonya watoto wao dhidi ya vitendo viovu kwa kuwafundisha maadili mema.

Sauti ya Mganga Mkuu wa halmashauri ya mji kasulu dokta, Peter janga

Baadhi ya wazazi katika halmashauri ya mji Kasulu wameiomba Serikali kuongeza Nguvu katika utoaji wa elimu kwa jamii,pamoja na kuwachukulia hatua baadhi ya wazazi watakao bainika kuwaficha wahalifu wa vitendo vya ukatili.