Joy FM

Ajeruhiwa kwa risasi vurugu zikiibuka baina ya polisi na wafugaji Uvinza

10 June 2024, 15:26

Kamanda wa jeshi la polisi Mkoani Kigoma SACP Filemon Makungu, Picha na Josephine Kiravu

Vurugu vimetokea baina ya jeshi la polisi mkoani kigoma na wafugaji hali iliyosababisha mto mmoja kujeruhiwa kwa kupigwa risasi.

Na Josephine Kiravu

Jeshi la Polisi mkoani Kigoma limethibitisha kutokea kwa vurugu baina ya askari polisi na wafugaji huko katika kijiji cha Mganza wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma ambapo mtu mmoja aitwaye Emanuel John alijeruhiwa kwa risasi mguu wa kushoto.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma SACP Filemon Makungu amesema tukio hilo limetokea Juni 07 ambapo askari polisi wakiwa doria walikutana na kundi la watu 10 wakiwa na ng’ombe 74 wanaodhaniwa wa wizi wakiwa wanasafirishwa bila kibali na wakati wa mahojiano na kundi hilo ndipo ziliibuka vurugu kwa askari kushambuliwa na silaha za jadi na mpaka sasa uchunguzi bado unaendelea.

Sauti ya Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Kigoma

Katika tukio lingine jeshi la polisi limethibitisha kutokea kwa ajali ya barabarani katika barabara ya Ikuburu eneo la Katare kijiji cha Rukoma kata ya Igalula wilaya ya Uvinza na kusababisha vifo vya watu watano na majeruhi watano.

Sauti ya kamanda wa polisi mkoani Kigoma

Hii si mara ya kwanza kutokea vurugu baina ya wafugaji na askari polisi katika wilaya ya Uvinza. Hata hivyo jeshi la polisi limeeleza kuhakikisha wanatokomeza matukio haya ambayo yamekuwa yakijitokeza huko Uvinza.