Serikali yapongezwa udhibiti, ramli chonganishi
29 May 2024, 09:55
Serikali wilayani kasulu imesema iitaendelea kuhakikisha ulinzi na usalama unaimarishwa kwa kuwachukulia hatua wale wote watakaoonyesha vitendo vya uvunjifu wa amani kwenye jamii ikiwemo ramli chonganishi.
Na Michael Mpunije – Kasulu
Madiwani katika halmashauri ya wilaya ya Kasulu Mkoani Kigoma wameipongeza kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya hiyo kwa namna ilivyoshughulikia na kufanikiwa kudhibiti suala la wapiga ramli chonganishi maarufu kamchape ambao wamekuwa wakisababisha uharibifu wa mali za wananchi.
Kudhibitiwa kwa kamchape ni kutokana na jitihada za kamati ya ulinzi na usalama wilayani Kasulu ambao wamehakikisha amani inatawala kwa raia ili kurahisisha kuendelea kufanyika shughuli za uzalishaji licha ya baadhi ya wananchi walionekana kuwaunga mkono waganga hao matapeli na kwa hivi karibuni hakujaripotiwa matukio ya kamchape katika wilaya hiyo kutokana na jitihada za jeshi la polisi kudhibiti matukio hayo.
Akizungumza mbele ya Mkuu wa wilaya ya Kasulu mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kasulu ambaye pia ni diwani wa kata ya kitanga bw.Elia kagoma mesema kwa sasa hali ni shwari ukilinganisha na miezi iliyopita.
Kwa upande wao baadhi ya madiwani katika halmashauri ya wilaya ya kasulu akiwemo diwani wa kata ya Bugaga Hitra Mlobelo ambaye kata yake ni miongoni mwa zilizoathiriwa na kamchape amesema kwasasa kata hiyo ina amani na wananchi wanaendelea na shughuli za maendeleo wakati huo diwani wa kata ya Asante Nyerere Julius Mpwehuka ameshauri kuendelea kufuatilia viashiria vya kamchape ili viweze kutokomezwa kabisa.