Joy FM

Wadau waombwa kusaidia wanafunzi walemavu

23 May 2024, 16:12

Mdau wa sekta ya elimu Mwalimu Yusuph Ibrahimu baada ya kutoa msaada kwa wanafunzi, Picha na Hagai Ruyagila

Jamii na wadau wa maendeleo wilayani Kasulu wametakiwa kujitoa kwa wanafunzi wenye ulemavu kwa kuwapa msaada wa mahitaji mbalimbali ili waweze kufikia malengo kama makundi mengine ya watoto.

Na Hagai Ruyagila – Kasulu

Wadau wa maendeleo katika wilaya ya Kasulu Mkoani Kigoma wametakiwa kuendelea kujitokeza kuwasaidia wananfunzi wenye ulemavu wa viungo ili kuwawezesha nyenzo mbalimbali zitakazowasaidia kusoma kwa urahisi na kufikia ndoto zao.

Rai hiyo imetolewa na mdau wa sekta ya elimu Mwalimu Yusuph Ibrahimu anayetokea shule ya msingi Kisuma iliyopo halmashauri ya wilaya ya Kasulu, baada ya kutoa msaada wa sare zashule kwa wanafunzi wenye uhitaji katika kituo cha watoto wenye mahitaji maalum kilichopo shule ya msingi Mwenge iliyopo kata ya Kumsenga halmashauri ya Mji Kasulu.

Sauti ya mdau wa elimu elimu kasulu Mwalimu Yusuph

Kwa upande wake mwalimu mkuu wa shule ya Msingi Mwenge Kevina Ndyana amempongeza mdau huyo wa elimu kwa namna anavyojitoa kutoa msaada kwa watoto wenye uhitaji.

Sauti ya mwalimu mkuu wa shule ya msingi mwenge kasulu

Aidha Mwalimu wa elimu maalum Loyce Kulinga kutoka kituo cha watoto wenye mahitaji maalum katika shule ya msingi Mwenge amesema watoto wengi wa jinsia ya kike wanakata tamaa na kushindwa kuendelea na masomo hivyo amewasihi wazazi na walezi kuendelea kuwatia moyo ili watoto hao waweze kuhitimu masomo yao vyema.

Sauti ya mwalimu wa elimu maalum Loyce Kulinga

Nao baadhi ya watoto hao wamemshukuru mdau huyo wa elimu kwa kuwapa zawadi hizo na kumuahidi kufanya vizuri katika masomo yao.

Sauti ya watoto wenye ulemavu
Wanafunzi wenye ulemavu wanaosoma katika shule ya msingi mwenge wilayani kasulu, Picha na Hagai Ruyagila

Kituo hicho cha watoto wenye mahitaji maalum kinapatika katika shule ya msingi Mwenge halmashauri ya Mji Kasulu kina jumla ya watoto 40 Wasichana 15 na Wavulana 25.