Joy FM

Serikali yagawa vifaa kwa shule zenye wanafunzi wa MEMKWA

17 May 2024, 14:41

Mkurugenzi wa halmashauri ya Mji Kasulu akikabidhi vifaa kwa wakuu wa shule zenye wanafunzi wa MEMKWA, Picha na Hagai Ruygaila

Serikali imesema itaendelea kushirikiana na wadau wa maendeleo katika kuhakikisha inaboresha elimu nchini kwa wanafunzi.

Na Hagai Ruyagila – Kasulu

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kasulu mkoani Kigoma Mwl. Vumilia Simbeye amekabidhi vifaa vya shule kwa wakuu wa shule 16 zenye wanafunzi wa MEMKWA lengo likiwa ni kuendelea kuwapa hamasa wanafunzi hao kusoma kwa bidii.

Akizungumza wakati wa zoezi hilo la ugawaji wa vifaa hivyo Mwl. Simbeye amesema halmashauri ya Mji Kasulu ina wanafunzi wa MEMKWA 644 ambao wapo katika shule za msingi 16 kati ya shule hizo zilizopo ndani ya halmashauri hiyo.

Mwonekano wa wanafunzi wakiwa darasani wakisikiliza jambo kutoka kwa mwalimu, Picha na Hagai Ruyagila

Mwl. Simbeye amewataka wakuu wa shule hizo kwenda kugawa vifaa hivyo kwa wanafunzi husika kama ilivyo kusudiwa na kwamba dhamira ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kuhakikisha kila mwanafunzi anapata elimu bora.

Sauti ya mkurugenzi wa halmashauri ya Mji wa Kasulu

Kwa upande wake Afisa Elimu Msingi halmashauri ya Mji Kasulu Julius Buberwa amemuahidi mkurugenzi wa halmashauri hiyo kuwa wataendelea kutekeleza wajibu wao katika kuwafundisha wanafunzi ili kuongeza ufaulu.  

Sauti ya afisa elimu msingi halmashauri ya mji Kasulu

Naye Afisa Elimu watu Wazima na elimu nje ya mfumo rasmi msingi halmashauri ya Mji Kasulu Felician Ferdinand amesema miongoni mwa vifaa vilivyotolewa na serikali ya Canada kupitia shirika la kuhudumia watoto duniani UNICEF ni pamoja na mabegi, madaftari na peni ambavyo vitawasaidia wanafunzi hao katika masomo yao.

Sauti ya afisa elimu watu wazima na elimu iliyopo nje ya mfumo rasmi wa elimu
Mkurugenzi wa halmashauri ya mji Kasulu akiwa katika halfa ya kukabidhi vifya kwa wakuu wa shule zenye wanafunzi wa MEMKWA, Picha na Hagai Ruyagila