Makanika atoa msaada kwa waathirika wa mafuriko
16 May 2024, 10:53
Serikali imesema itaendelea kuwasaidia wananchi walipata madhara ya nyumba na mali zao kuharibika kufuatia mvua zilizonyesha na kuacha simanzi kwa wananchi katika vijji vya jimbo la kigoma kaskazini ikiwemo pamila, nyarubanda na mwamgongo.
Na Tryphone Odace – Kigoma Dc
Wananchi wa vijiji cha Pamila na nyarubanda katika halmashauri ya wilaya Kigoma wameiomba Serikali kuona namna ya kuwasiadia kwani wengi wao bado hawana sehemu za kuishi baada ya nyumba zao kubomoka kufuatia mvua zilizokuwa zinanyesha mwezi machi mwaka huu.
Wametoa ombi hilo mara baada ya Mbunge wa Jimbo la Kigoma kaskazini Mh Assa Makanika kutembelea kaya zilizoathirika na mvua hizo na kuwapatia misaada ya vitu mbalimbali ikiwemo vyakula.
“kwa tunaishi maisha magumu hatuna kitu wazazi wangu wanaishi kwenye nyumba za kupanga ambazo pia nazo sio imara na hatujui hatima yetu maana hata mazao shambani walipelekwa na mvua mashamba niombe serikali ingeangalia vizuri namna ya kutusaidia.”
Naye Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi wilaya ya Kigoma Almashi Mayonga amesema wao kama chama wataendelea kuhakikisha serikali inawafikia wananchi Kwa kufikisha huduma muhimu za kijamii.
Kwa upande wake, mbunge wa Jimbo la Kigoma kaskazini Mh. Assa Makanika amesema kupitia kamati ya maafa ya halmashauri walipokea kaya zilizoathirika na mvua na kuamua kuja kuwatembelea na kuwasiadia kama sehemu ya kuunga Mkono juhudi za Rais katika kuhakikisha wanainua maisha ya wananchi.