Joy FM

UNHCR na tanzania zatoa msimamo kwa wakimbizi wa burundi.

13 May 2024, 15:41

Wakimbizi wanaoishi katika kambi ya Nduta wilayani kibondo, Picha na Lucas Hoha

Wakimbizi wa nchi ya burundi wanaohifadhiwa mkoani Kigoma, wametakiwa Kurejea Nchini Burundi mara moja ili kuungana na ndugu zao kujenga Taifa hilo,  kabla ya kufutiwa hadhi ya Ukimbizi  na kukosa misaada ya Kibinadamu ifikapo Mwezi Desember Mwaka huu.

Na, Lucas Hoha – Kibondo

Baadhi ya wakimbizi na waomba hifadhi kutoka nchini Burundi waliopo katika kambi ya wakimbizi nduta iliyopo Wilaya ya Kibondo Mkoani Kigoma wamesema wako tayari kurudi nchini  mwao kwa hiyari huku nawakiomba serikali ya Tanzania na mashirika ya kimataifa ikiwemo UNHCR kuweka mazingira wezeshi ya wao kurudi nchini mwao.

Wamesema hayo mara baada ya mkutano uliofanyika kambini hamo uliowakutanisha baadhi ya viongozi wa wizara ya mambo ya ndani nchini Tanzania na baadhi ya viongozi wa mashirika ya kimataifa yanayohudumia wakimbizi ikiwemo UNHCR katika mkutano uliobeba ujumbe wa kuwaomba wakimbizi hao kurundi nchini burundi.

Sauti ya wakimbizi wanaohifadhiwa katika kambi ya Nduta kibondo

Mkurugenzi wa idara ya huduma kwa wakimbizi kutoka wizara ya mambo ya ndani nchini Tanzania Sudi Mwakibasi amesema wakakubali  kurudi kwao  kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kuwepo kwa ongezeko la watu wenye uhitaji duniani kwa sababu ya mabadiliko ya tabia nchi, athari za Uviko 19 na majanga ya vita hivyo mashirika ya kimataifa kushindwa kutoa msaada wa ufanisi kambini hapo.

Mkurugenzi wa idara ya wakimbizi kutoka wizara ya mambo ya ndani, Picha na Lucas Hoha
Sauti ya mkurugenzi wa idara ya wakimbizi

Kwa upande wake, Afisa uhifadhi wakimbizi msaidizi kutoka Ofisi ndogo ya shirika la kuhudumia wakimbizi Duniani UNHCR Wilaya ya Kibondo Sabina Luoga amesema hatua ya wakimbizi wa Burundi kurejea kwao kwa hiari nimakubaliano  ya serikali ya Tanzania, mashirika ya Kimataifa ya hudumia wakimbizi na Serikali ya Burundi yaliyofanyika Novemba 2023, na kuwa serikali ya Burundi imekubali kuwapokea watu wake na kuandaa mazingira wezeshi ya kuishi.

Sauti ya afisa uhifadhi wakimbi UNHRC ofisi ya kibondo

Zaidi ya wakimbizi laki moja 100,000 kutoka Jamhuri ya Burundi wamesharejea nchi kwao tangu serikali na mashirika ya kimataifa yaanze kampeni ya kuwahamasisha wakimbizi hao kurejea kwa hiari.