Vijana wa JKT kutumika katika uzalishaji mali
8 May 2024, 14:26
Vijana wanaomaliza mafunzo ya kijeshi wametakiwa kuendelea kutumia ujuzi wa uzalishaji mali ili kusaidia kuzalisha na kuwa mstari wa mbele katika kulinda amani.
Na Kadislaus Ezekiel – Kakonko
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jocob Mkunda, amewataka vijana wanaohitimu mafunzo ya kijeshi nchini kutumia elimu wanayopewa vikosini, kusaidia taifa kuongeza uzalishaji mali hasa katika sekta ya kilimo na kuwa mstari wa mbele kujiepusha na uvunjifu wa amani.
Katika taarifa yake Jenerali Mkunda iliyosomwa na Mkuu wa Tawi la Lojistiki na Uhandisi Jeshini, Meja Jeneral Hawa Kodi wakati wa kufunga mafunzo ya Oparesheni miaka sitini ya JKT katika kambi ya 824KJ KANEMBWA Kakonko, amewataka wahitimu wa mafunzi ya Kijeshi kuwa chachu ya uzalishaji mali.
Awali Akitoa taarifa ya Kuhitimu mafunzo kwa vijana OPARESHENI Miaka sitini ya Jeshi la Kujenga Taifa, Kamanda kikosi 824 KJ KANEMBWA Luteni Kanal Mantange Nkombe, amesema Vijana wamefanikiwa kwa viwango vinavyokubalika ndani ya Jeshi la kujenga Taifa, wakati Vijana wakieleza kutumia mafunzo, katika kusaidia jamii katika majanga.
Mafunzo hayo yamefungwa na Mkuu wa Wilaya ya Kakonko, Kanali Evance Malasa na kusisitiza Vijana kujiepusha na matumizi ya mitandao katika kufanya uhalifu.