Joy FM

RC Kigoma awataka vijana kutumika kimaendeleo

3 May 2024, 14:00

Mkuu wa mkoa wa Kigoma Kamishna Jenerali mstaafu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye ameiasa jamii kutumia nguvu kazi ya vijana katika shughuli za Kimaendeleo ili kuongeza uchumi wa taifa na jamii kwa ujumla.

Ametoa wito huo wakati akizungumza na watumishi wa sekta ya Umma na taasisi binafsi kutoka katika wilaya tano zilizopo mkoani Kigoma   pamoja baadhi ya wananchi wa wilaya ya kasulu katika uwanja wa umoja uliopo halmashauri ya Mji Kasulu.

Andengenye amesema ni vizuri jamii kutumia nguvu kazi ya vijana iliyopo hapa nchini kwani ni kundi ambalo linaweza kukabiliana na shughuli za kimaendeleo ili kuweza kujiingizia kipato.

Mkuu wa Mkoa Kigoma: Mh. Thobias Andengenye

Aidha Andengenye amesisitiza kufanya mapinduzi ya kifikra na kimatendo yatakayosaidia kupiga hatua ya kimaendeleo kwa mwananchi mmoja mmoja katika kuongeza bidii ya kazi ili kupata mafanikio zaidi ya kiuchumi.

Mkuu wa Mkoa Kigoma: Mh. Thobias Andengenye

Kwa upande wao wananchi mkoani Kigoma akiwemo Ishimie Danford, Enos Chesa na Goerge Mamboleo wamesema jamii ikiwawezesha vijana itasaidia kwa kiasi kikubwa taifa kuwa na maendeleo makubwa maana vijana wengi hawana kazi za kujiingizia kipato licha ya elimu walizonazo.

wananchi