Joy FM

Wananchi wajenga shule kunusuru watoto wao na mimba

2 May 2024, 17:02

Mkuu wa wilaya Buhigwe akiwa na wananchi wakijitolewa kujenga shule, Picha na Tryphone Odace

Serikali imesema itaendelea kusaidiana na wananchi katika kuhakikisha wanafanikisha utoaji wa huduma muhumu ikiwemo kujenga shule ili kutatua changamoto za wanafunzi kutembea umbali mrefu kutafuta elimu katika kijiji kingine.

Na Michael Mpunije – Buhigwe

Wananchi wa kijiji cha Nyankoronko kata ya Buhigwe wilayani Buhigwe mkoani Kigoma wameanzisha ujenzi wa shule ya sekondari katika kijiji hicho ili kuondoa usumbufu wa wanafunzi kufuata Elimu katika shule ya Sekondari Buyenzi ambayo ipo umbali wa Zaidi ya kilimota 5 kutoka katika kijiji hicho.

Ujenzi wa shule hiyo mpya umetokana na wanafunzi kusafiri umbali mrefu ambapo katika kipindi cha masika wanafunzi wanachelewa kufika shule wakati mwingine kunyeshewa na mvua.

Jenesia nfatiye,Jonas kalaheze na kezia nzogera ni baadhi ya wananchi wa kijiji cha nyankoronko ambao wameomba serikali kuunga mkono ujenzi wa shule hiyo .

Sauti ya wananchi kijiji cha nyankronko na ujenzi wa shule

Mkuu wa wilaya ya Buhigwe kanali Michael ngayalina akizindua ujenzi wa shule mpya ya nyankorongo amesema serikali itahakikisha inawaunga mkono wananchi katika ujenzi huo hasa watakapofikia hatua ya boma na kwamba wanafunzi wataondokana na adha ya kufuata ELIMU umbali mrefu.

Dc ngayalina na wananchi wakikusanya tofali kwa ajili ya kujenga shule
Sauti ya Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe kanali ngayalina

Aidha kanali Ngayalina ametoa mifuko 20 ya saruji kwa ajili ya kuongeza nguvu katika ujenzi huo na kuwataka wananchi kuepuka migogoro ili kuwa na umoja katika ujenzi wa mradi huo wa shule.

Sauti ya kanali ngayalina mkuu wa wilaya buhigwe

Kwa mjibu wa mtendaji wa kijiji hicho akiwasilisha taarifa ya fedha za wananchi zilizokusanywa kwa ajili ya ujenzi wa shule hiyo mpya ya sekondari ni jumla ya shilingi milioni 3laki 9 na elfu 17 na wameanza na ujenzi wa madarasa mawili na ofisi moja.

Mkuu wa wilaya ngayalina akizungumza na wananchi