Saratani ya mlango wa kizazi inatibiwa acheni imani potofu
22 April 2024, 09:30
Ugonjwa wa Saratani ya mlango wa kizazi kwa watoto wa kike imeendelea kuwa tatizo jambo ambalo limeiamsha serikali kuendelea na kampeni ya chanjo kwa watoto wa kike ili kuepukana na ugonjwa huo
Na Emmanuel Kamangu – Buhigwe
Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe Mkoani Kigoma wanatarajia kutoa chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi kwa mabinti elfu 23,982 wenye umri wa kuanzia miaka 9 hadi 14
Akizungumza na Redio Joy, Mratibu wa huduma za chanjo Wilaya ya Buhigwe Stepphano Mambula amesema zoezi hilo linatarajiwa kuanzia tarehe 22 hadi 24 lengo ikiwa ni kukabiliana na ugonjwa wa saratini ya mlango wa kizazi kwa mabinti wa kike.
Bw.Mabula amesema kwa kiasi kikubwa chanjo zinazoendelea kutolewa zimekuwa msaada mkubwa katika kuwakinga mabinti na maambukizi hasa kwenye via vya uzazi hivyo kuwataka wazazi kutowaficha wakati zoezi la chanjo litakapokuwa likiendelea.
Kwa upande wao baadhi ya wananchi wa Wilaya ya buhigwe wameishukuru serikali kupitia idara ya afya kwa chanjo mbalimbali ambazo zimekuwa zikitolewa kwa mabinti kwani zimekuwa msaada mkubwa katika kukabiliana na magonjwa mbalimbali ikiwemo ya uzazi.