Akutwa amefariki bwawani Kigoma
15 April 2024, 15:29
Wananchi wakawa pembezone mwa bwawa la Katubuka kushuhudia mwili wa mtu aliyetwa amefariki
Wananchi wameomba Serikali ya Mkoa wa Kigoma kwasaidia wananchi kuchukua hatua dhidi ya bwawa la Katubuka ambalo limeendelea kuchukua maisha ya watu kutokana na maji kuja na wananchi kukosa njia ya kupita
Na Kadislaus Ezekiel
Mtu Mmoja ambaye hakutambulika majina yake, amekutwa amefariki katika bwawa la Katubuka Manispaa ya Kigoma Ujiji, eneo ambalo limejaa maji kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha na kuzua taharuki kwa wananchi huku wakipaza Sauti kwa Serikali kuchukua hatua kuondoa maji yanayozidi kuvamia makazi.
Baadhi ya Mashuhuda wakizungumza kwa masikitiko kufuatia kifo hicho, wameomba Serikali ichukue hatua kuondoa maji katika eneo la Katubuka ili kuepusha maafa kuendelea kutokea.
Diwani wa Kata ya Katubuka Moshi Mayengo, Ameomba Serikali kupitia kamati ya maafa kufanya uchunguzi kuondoa maji ya katubuka ili kuepusha maafa kuendelea kutokea kwa wanachi.
Kaimu Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokozi Mkoa wa Kigoma Inspekta Jacobu Chacha amesema chanzo cha kifo hicho ni baada ya marehemu kutumbukia kwenye bwawa la Katubuka,na kwamba kifo hicho ni cha kwanza kutokea tangu wananchi kuvamiwa na maji.