Wanafunzi kuchukuliwa hatua matumizi ya madawa ya kulevya Kigoma
5 April 2024, 14:11
Wanafunzi mkoani Kigoma wametakiwa kuacha kutumia madawa ya kulevya na endapo atabainika yeyote anayetumia taarifa zitolewe kwa viongozi wao ili achukuliwa hatua za kisheria.
Hayo yamebainishwa na Mdhibiti Ubora wa Shule halmashauri ya wilaya ya Kigoma Gibson Ntamamilo wakati wa kongamano la Ukwata lililofanyika katika shule ya sekondari Mikamba iliyopo kata ya Kidahwe.
Mwalimu Ntamamilo amesema wapo baadhi ya wanafunzi wanatumia na kujihusisha na vitendo visivyofaa katika jamii ni vizuri kuacha ili kuwa na tabia njema.
Pia Mwalimu Ntamamilo amesema ni vizuri kuulinda utamaduni uliopo katika nchi ya Tanzania kuliko kuwa balozi kwa mafundisho na vitendo visivyofaa ndani ya jamii yao.
Kwa upande wake Mchungaji mratibu wa Ukwata mkoa wa Kigoma Salvatory Jeremiah amesema baadhi ya wanafunzi wengi waliopo shuleni wanashindwa kuzingatiwa malengo yaliyowapeleka shule na kujikuta wanatumia madawa ya kulevya.
Nao baadhi ya wanafunzi wa ukwata mkoa wa kigoma ambao wameshiriki katika kongamano hilo wamesema madawa ya kulevya yana madhara makubwa kwa mwanadamu hali inayopelekea kupoteza nguvu kazi ya taifa.