Mapato yapotea, chanzo kukosekana kwa POS Kasulu
5 March 2024, 10:09
Kukosekana kwa mtambo wa ukusanyaji wa mapato (POS) Personal Operating System kwa baadhi ya kata ikiwemo Nyumbigwa na Murufyiti zilizopo halmashauri ya Mji kasulu Mkoani Kigoma imepelekea halmashauri hiyo kuendelea kupoteza mapato
Hayo yamebainishwa na Watendaji wa kata hizo mbili ambao ni afisa mtendaji wa kata ya Nyumbigwa Francis Jeremea na afisa mtendaji wa kata ya Murufiti Nasibu Rashidi Kasunzu wakati wa kusoma taarifa za kata hizo katika kikao cha baraza la madiwani kilichofanyika katika ukumbi mkubwa wa halmashauri ya Mji Kasulu Mkoani Kigoma.
Wamesema kukosekana kwa kifaa hicho imepelekea kushindwa kukusanya mapato licha viongozi wa kata hizo kutoa elimu ya kodi lakini ukusanyaji wa mapato ndio changamoto hali inayopeleka kupoteza mapato ya halmashauri.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya Mji Kasulu Julius Buberwa amekiri kwa baadhi ya kata kutopelekewa mtambo huo wa ukusanyaji wa mapato.
Naye afisa biashara wa Halmashauri ya Mji Kasulu Joseph Simbila amesema tayari wametoa oda ya kununua mitambo hiyo na hivi karibuni watendaji ambao hawana mitambo hiyo watapewa ili kuanza ukusanyaji wa mapato