kamchape wahatarisha usalama Kasulu
28 February 2024, 09:45
Kufuatia uwepo wa migogoro ya ardhi na suala la ramli chonganishi inayofanywa na watu wanaojiita Kamchape katika kata ya Mganza iliyopo halmashauri ya Mji Kasulu Mkoani Kigoma imepelekea suala la ulinzi na usalama kuwa changamoto katani humo.
Afisa mtendaji wa kata ya Mganza Bw. Benedictor Makoye amebainisha hayo wakati akiwasirisha taarifa ya kata hiyo katika kikao cha baraza la madiwani cha robo ya pili ya mwaka.
Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa halmashauri ya Mji Kasulu Seleman Kwilusha amesema serikali imeshaandaa mpango wa kutatua changamoto hizo ili kata iwe salama.
Naye katibu tawala wa wilaya ya Kasulu Bi. Theresia Mtewele amesema serikali haitavumilia vitendo vya namna hiyo vikiendelea kufanyika na badala yake amewaagiza Watendaji wa kata na Madiwani kuhakikisha wanashughulikia changamoto hizo