KUWASA yabaini michezo michafu kwenye mita za maji
23 February 2024, 16:03
Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Manispaa ya Kigoma Ujiji KUWASA imekemea tabia ya baadhi ya wananchi wanaoharibu miundombinu ya maji kwa kukata mabomba ya maji na wengine kuiba mita za maji.
Na, Lucas Hoha
Akizungumza na Joy Fm, Meneja wa Wakala wa Maji Safi na Usafi wa Mazingira KUWASA Manispaa ya Kigoma Ujiji, Mhandisi Poas Kilangi amesema wananchi wanapoharibu miundombinu ya maji wanarudishia nyuma juhudi za mamlaka kuwahudumia wananchi, huku akianisha baadhi ya adhabu ambazo mwananchi atakumbana nazo pindi anapokamatwa akifanya uharibifu huo.
Aidha kilangi anasema suala la wizi wa mita za maji limeendelea kupungua katika manispaa hiyo na hii imetokana na ushirikiano walioupata kutoka kwa jeshi la polisi pamoja na wananchi, na kuwa wananchi wanaoiba mita hizo wanaziuza kama chuma chakavu.
Nao baadhi ya wananchi wamesema uharibifu wa miudnombinu ya maji katika manispaa hiyo ni wa muda mrefu huku wakiomba wananchi wenye tabia hizo kuziacha.
Elimu inatakiwa kuendelea kutolewa kwa wananchi kuhusu uharibifu wa miundombinu ya maji kwani wapo baadhi ya wananchi wanaokata mabomba ya maji kwa kujua au kutokujua kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo shughuli za kilimo na uborshaji wa miundombinu ya barabara.