Idadi ya wanafunzi walioripoti shule Kasulu hairidhishi
20 February 2024, 11:25
Tangu shule zifunguliwe januari 8 mwaka 2024 takwimu zinaonyesha wanafunzi walio wengi hawajaripoti kuanza masomo ya kidato cha kwanza.
Na Michael Mpunije
Idadi ya wanafunzi walioripoti shuleni kuanza kidato cha kwanza tangu shule zilipofunguliwa januari 8 mwaka huu inatajwa kuwa ndogo kwa baadhi ya shule za sekondari katika halmashauri ya wilaya ya kasulu mkoani Kigoma kutokana na mwamko mdogo wa elimu kwa baadhi ya wazazi na walezi wilayani humo.
Hayo yameelezwa na katibu tawala wilaya ya kasulu Bi,Theresia mtewele wakati akizungumza na madiwani wa kata mbalimbali za halmashauri ya wilaya ya kasulu akiwataka kushirikiana na watendaji wa kata kuhakikisha watoto wote waliochaguliwa kuanza kidato cha kwanza wanaripoti shuleni.
Bi,mtewele mesema kuwa serikali imeboresha miundombinu ya elimu ili kuhakikisha wanafunzi wanapatiwa elimu bora itakayo wasaidia katika maisha yao ya baadae.
Aidha katika hatua nyingine Bi,Mtewele amewataka madiwani kusimamia kikamilifu fedha za serikali zinazotolewa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo ili ziweze kuleta tija kwa wananchi.