uwepo wa masoko ya uhakika kutatua changamoto za wakulima
16 February 2024, 15:31
Wakulima Katika Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma, wameiomba Serikali kusaidia upatikanaji wa soko la uhakika la kuuza mazao ya mahindi na maharage, kufuatia ongezeko kubwa la uzalishaji wa mazao hayo, ikiwa ni baada ya kupatiwa mbinu za uzalishaji wenye tija.
Wakulima hao Wamesema hayo, wakati wa mdahalo wa siku ya mkulima, chini ya mradi wa kilimo tija Kigoma TIKITI, unaofadhiliwa na shirika la world vision na goodneighbours chini ya serikali ya korea na kutathimini hali ya uzalishaji wa mazao hasa mahindi na maharage.
Kwa upande wake meneja mradi wa kilimo tija Kigoma TIKITI, kutoka shirika la world vision Acquiline Wamba amesema mradi, unalenga kuwafikia wakulima zaidi ya elfu ishirini na kuwawezesha kulima kilimo biashara.
Aidha akizungumzia suala la Masoko kwa wakulima Katibu tawala wa Wilaya ya Kakonko Mauridi Mtulia akiwataka wakulima kuwa katika vyama vya ushirika ili kurahisisha ununuzi wa mazao..