Kigoma: Wananchi waonywa matumizi ya dawa kiholela kutibu macho mekundu
8 February 2024, 19:59
Wananchi mkoani Kigoma wametakiwa kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa macho mekundu, ulioripotiwa hivi karibuni kutokea katika baadhi ya mikoa mbalimbali hapa nchini.
Na, Horida Sayoni
Mganga mkuu wa mkoa wa kigoma Dr. Jesca Leba Amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari, ambapo amekiri tayari kesi kadhaa za ugonjwa zimekwisha ripotiwa katika ofisi yake na kwamba wengi wao tayari wamepata nafuu.
Dr. Jesca Amesema wanaendelea kutoa elimu kwa wananchi ili kuepusha maambukizi zaidi ya ugonjwa huo ambao hupelekea baadhi yao kupata uoni hafifu au kupoteza kabisa uwezo wa kuona Huku akiwataka wananchi kuacha tabia ya kutumia dawa kiholela na badala yake wafike kwenye vituo vya Afya ili kupata huduma stahiki na kudumisha usafi
Kwa upande wao Baadhi ya wananchi Abdallah Juma na Said mohamed wamesema kuwa elimu iendelee kutolewa ili kuwaepusha na ugonjwa huo wa macho mekundu.