Kigoma: Miradi ya kimkakati kuimarisha uchumi nchini, nchi jirani
1 February 2024, 10:49
Serikali imesema inaendelea kuhakikisha inaboresha miradi ya kimkakati kwenye sekta ya usafiri iliyopo ili kusaidia katika ukuaji wa uchumi hasa kupitia sekta ya usafirishaji kwa njia ya maziwa.
Na, Tryphone Odace.
Meneja Mipango kutoka kampuni ya huduma za meli nchini (MSCL) Mhandisi Gaspar Semoka amesema hayo baada ya kutembelea bandari ya Kigoma ili kujionea ukarabati na matengenezo unaoendelea kwenye meli zitakazofanya safari zake ndani ya ziwa Tanganyika.
Aidha amesema ipo miradi mingine ambayo inaendelea kutekelezwa ili kuhakikisha huduma za usafiri kwa njia ya maji zinarejea zikiwa imara.
Kwa upande wake, Msimamizi wa mradi wa ukarabati wa meli ya mafuta Mt. Sangara Mhandisi Kariuki Njenga amesema mradi wa ujenzi wa meli hiyo umefikia alimia 92 na ikikamilika itaanza kutoa huduma haraka.