Joy FM

Nyamori kupata shule ya sekondari kwa mara ya kwanza

1 February 2024, 10:11

Wananchi wa kijiji cha Nyamori kata ya Simbo katika wilaya ya Kigoma  wameipongeza serikali kwa juhudi za uboreshaji wa miundombinu ya elimu hasa ujenzi wa shule katika maeneo mbalimbali mkoani Kigoma.

Wameeleza hayo wakati wakipokea mifuko 50 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa shule mpya ya sekondari Nyamori kijijini hapo ikiwa ni moja ya utekelezaji wa mradi wa maendeleo ya elimu na hapa wanaeleza.

 Mwenyekiti wa wa kijiji cha Nyamori Bw.Thomas Kibirith Mvutelo akaeleza changamoto ya kuwalipa vibarua katika ujenzi wa shule hiyo na kuiomba serikali kupitia mkuu wa wiliya Mh. Salum Kali kuweza kutatua changamoto hiyo.

Naye Afisa Elimu Sekondari wilaya ya Kigoma Exavery Ntambala amewataka wananchi katika  wilaya ya kigoma kushiriki katika uboreshaji wa miundombinu ya elimu ili kusaidia watoto kuepuka kutembea umbali mrefu kufata huduma ya elimu.

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya kigoma Mh. Salum Kali wakati akikabidhi mifuko ya saruji iliyotolewa na wadau wa elimu ameahidi kusimamia na kutoa ushirikiano kwa wananchi kuhakikisha ujenzi wa shule wa Sekondari Nyamori unakamilika.