Bilioni 3 kujenga ofisi mpya za wilaya Kibondo
25 January 2024, 15:16
Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo Mkoani Kigoma imeanza ujenzi wa ofisi mpya za halmashauri hiyo zitakazogharimu zaidi ya shilingi bilioni 3 mpaka kukamilika kwake ikiwa ni mikakati ya serikali ya kuboresha mazingira ya kutolea huduma kwa wananchi.
Na, James Jovin
Hayo yamebainishwa na Kaimu Afisa mipango wa halmashauri ya wilaya ya Kibondo Daniel Ndarangavye akimwakilisha mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo katika ziara ya kitaifa ya jumuiya ya umoja wa vijana ccm.
Kwa upande wake, kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Kibondo Steven Janks amesema kuwa ujenzi wa jengo hilo mpaka sasa umefikia asilimia arobaini na kwamba tayari zimepokelewa fedha shilingi bilioni 2 kwa ajili ya kuendelea na utekelezaji.
Naye kaimu mwenyekiti wa jumuiya ya umoja wa vijana cmm taifa bi. Rehema Sombi amemshukuru raisi Samia Suluhu Hassani kwa kutenga fedha za ujenzi wa jengo hilo ambalo litakuwa na manufaa makubwa kwa wananchi wa wilaya ya Kibondo.