Kibondo: Vijana waaswa kutumia amani iliyopo kusoma kwa Bidii
25 January 2024, 11:22
Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Taifa Rehema Sombi, amewataka vijana wa kitanzania kutumia amani iliyopo kusoma kwa juhudi na maarifa ili kuhakikisha nchi inapiga hatua zaidi kimaendeleo kwa kuwa na watu wenye uwezo wa kukabili changamoto za kimaisha.
Amesema hayo baada ya kutembelea na kukagua madarasa mapya na bweni yaliyojengwa na serikali kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo katika shule ya sekondari ya wasichana ya Kibondo katika mwendelezo wa ziara ya viongozi wa UVCCM Taifa mkoani Kigoma inayolenga kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Amesema Rais Samia Suluhu Hassan na wasaidizi wake serikalini wameendelea kuboresha miundombinu hususan katika kujega vyumba vya madarasa, kuajiri walimu na kuhakikisha elimu inapatikana bila malipo kuanzia kidato cha kwanza hadi kitado cha sita.
Kwa upande wao wanafunzi wa shule ya sekondari Kibondo wameishukuru serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuboresha miundombinu ya kujifunzia katika skuli hiyo na kuwawezesha kusoma katika mazingira mazuri.