Michango mingi yawaondoa walimu CWT
22 January 2024, 12:30
Baadhi ya waalimu wilayani Kasulu Mkoani Kigoma wameulalamikia uongozi wa chama cha walimu Tanzania (CWT) kwa kuwakata michango mingi hali inayopelekea baadhi ya waaalimu kijiondoa katika chama hicho.
Akizungumza katika kikao cha wadau Elimu Mkuu wa shule ya sekondari Ruchugi kata ya Msambala halmashauri ya Mji Kasulu Mwalimu Greson Zize amewaomba viongozi wa chama hicho kupunguza michango kwa wanachama ili kunusuru walimu kujiondoa kwenye chama hicho.
Amesema kutokana na wingi wa michango hiyo baadhi ya viongozi wamekuwa wakikataa nafasi walizoteuliwa kwa kuepuka lawama kutoka kwa baadhi ya waalimu.
Mwenyekiti wa chama cha walimu wilayani kasulu Mwalimu Elisha Kebelo amesema makato hutokana na mshahara anaoupokea mwalimu husika na kuahidi kulifanyia kazi katika mkutano wao ujao.
Kwa upande wake Waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu kazi, vijana, ajira na wenye ulemavu ambaye ni mbunge wa Jimbo la Kasulu mjini Mhe, Prof Joyce Ndalichako amesema utatuzi wa changamoto hiyo uko ndani ya mamlaka ya chama husika.