TRA Kasulu yashindwa kufikia malengo
22 January 2024, 09:20
Mamlaka ya mapato Tanzania TRA wilaya ya Kasulu mkoani kigoma imeshindwa kufikia lengo la ukusanyaji mapato katika kipindi cha mwezi julai hadi Desemba 2023 ikiwa ni nusu ya bajeti ya mwaka wa fedha 2023/2024.
Na, Hagai Ruyagila
Akitoa taarifa katika Kikao cha kujadili mapendekezo ya mpango na bajeti ya mapato na matumizi pamoja na miradi ya maendeleo kwa mwaka 2024/ 2025 halmashauri ya wilaya ya Kasulu Meneja wa TRA wilaya Luis Odhiambo amesema kuwa mamlaka hiyo imefanikiwa kukusanya mapato kwa asilimia 98 pekee ya mapato .
Odhiambo amesema lengo ilikuwa kukusanya kiasi cha shilling billion 2 million 301 laki 679 elfu lakini zimekusanywa billion 2 million 260 laki 697 elfu na mia 917.45 na kwamba wameshindwa kufikia lengo kutokana na utayari mdogo wa ulipaji kodi kwa baadhi ya wafanya biashara.
Kwa upande wake mwenyekiti wa chama cha mapinduzi wilaya ya Kasulu Mberwa chidebwe ameishauri TRA kwa kushirikiana na halmashauri kuweka utaratibu mzuri wa ukusanyaji mapato ili kuzuwia upotevu wa pesa ambao umekuwa ukijitokeza .
Naye Andrew Stanley Ching’ole Muwakilishi kutoka shirika la UNHCR amesema ni vizuri kutengeneza vyanzo vingi vya mapato ya ndani ili kusaidia kupata mapato mengi yatakayoweza kusaidia kujiendesha wenyewe kuliko kutegemea serikali kuu.