Polisi Kigoma yakamata silaha 16 zinazomilikiwa kinyume na sheria
15 January 2024, 13:23
Jeshi la Polisi Mkoani kigoma limefanikiwa kukamata silaha 16 zilizokuwa zinamilikiwa kinyume na sheria huku washatakiwa 2 wa kesi za kupatikana na hatia wakihukumiwa kifungo cha kwenda jela miaka 20 kila mmoja baada ya kupatikana na hatia ya kumiliki silaha aina ya gobore kinyume na sheria.
Na Josephine Kiravu.
Kamanda wa polisi mkoani Kigoma ACP Filemon Makungu amesema hayo katika mkutano na wanahabari ofisini kwake wakati akieleza mafanikio ya misako na operesheni mbalimbali zinazoendelea katika wilaya zote za mkoa wa kigoma.
Katika hatua nyingine Kamanda makungu amesema katika kuzuia ajali za barababarani kwa kipindi cha kuanzia mwezi Januari hadi Disemba 2023 jumla ya makosa 62,917 ya usalama barabarani yamekamatwa na kutozwa faini.
Kwa upande wa dawa za kulevya Mahakama ya wilaya ya kasulu imemhukumu kifungo cha kwenda jela kwa miaka 50 mshatakiwa mmoja wa kesi ya kulima dawa za kulevya aina ya bangi.
Hata hivyo jeshi la polisi limewaomba wananchi kuendelea kushirikiana na jeshi hilo katika kuzia na kubaini uhalifu na uhalifu kwa lengo la kuimarisha usalama wa raia na mali zao.