Joy FM

Zaidi ya nyumba 100 zaezuliwa wilayani Kibondo

15 January 2024, 11:49

Tathimini iliyofanywa na kamati ya maafa wilayani Kibondo mkoani Kigoma imebaini kuwa zaidi ya nyumba 100 ziliezuliwa na mvua iliyoambatana na upepo katika kambi ya wakimbizi Nduta ndani ya wiki mbili zilizopita.

Hayo yamebainishwa na mkuu wa wilaya ya Kibondo kanali Agrey Magwaza wakati akizungumza na radio Joy ofisini kwake na kwamba mtoto mmoja pia alifariki dunia kwa kusombwa na maji katika mifereji ya maji iliyoko kambini humo

Aidha kanali Magwaza amesema kuwa zaidi ya watu 14 walijeruhiwa kutokana na kuangukiwa na miti iliyoangushwa na upepo ndani ya kambi hiyo na hivyo kusababisha madhara katika baadhi ya familia.

.